Na Sophia Kingimali
SHIRIKA
inayoshughulikia walemavu wa ngozi Under the same sun (UTSS)
ikishirikiana na Serikikali ya Canada kupitia ubalozi wake nchini
Tanzania imeanzisha mradi wa redio katika kanda ziwa.
Mradi huo umezinduliwa leo jijini Dar es salaam na hafisa mradi bi
Rachel Moyoikiwa na lengo la kuelimisha jamii na kuongeza uelewa kwa
jamii kuhusu albinism.
Aidha Moyo amesema kuwa watatumia redio za kijamii zilizopo kanda ya
ziwa kuendesha vipindi katika mtindo wa makala mchanganyiko,majadiliano
ya moja kwa moja pamoja na mchango wa simu kutoka kwa wasikilizaji na
pia michezo ya kuigiza.
"Jopo la majadiliano la moja kwa moja ambalo litaendeshwa ni pamoja
na mazungumzo kati ya watu wenye albinism na wataalamu wa maswala ya
albinism ikiwa ni pamoja na michango ya wasikilizaji kwa njia ya simu"
alisema Moyo.
Moyo ameongeza kuwa redio zitakazoendesha vipindi vya “tambua
albinism”ni pamoja na Sengerema Fm,Sibuka Fm,Faraja Fm,Fadeco Fm,Kahama
Fm na Chemchem Fm pia ametoa wito kwa redio ambayo itakayo kuwa tayari
kushiriana nao wataipa ushirikiano.
via: http://www.habarimpya.com
Loading...
Post a Comment