Loading...

JAJI MSTAAFU MH. ERNEST MWAIPOPO AFARIKI DUNIA KWA AJALI

Mrehemu Jaji Mstaafu Mh. Ernest Mwaipopo                   
 
JAJI MSTAAFU Mh. ERNEST MWAIPOPO amefariki katika ajali iliyotokea mkoani morogoro leo alipokuwa akirejea Dar es Salaam kutokea Mkoani Iringa. 

Hayo yameelezwa na mtoto mdogo wa marehemu Lukelo Mkami  Mwaipopo  alipozungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin. blogspot.com ambapo amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo wakati  akitokea  mkoani Iringa.

Lukelo amesema  kuwa katika gari  hiyo  walikuwepo  watu  watano pamoja na dereva na  kuwa chanzo  ajali hiyo kinatajwa  kuwa ni kupasuka kwa taili la mbele .

Hata  hivyo alisema  kuwa  taratibu  za mazishi zitafahamika baada ya mwili  huo kupelekwa  jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya taratibu  za mazishi yatakayofanyika katika wilaya ya Mufindi.
Chanzo: Francis Godwin Godwe Mzee wa Matukio DaimaPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top