Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA imetangaza viwango vipya vya nauli za mabasi ya masafa marefu, daladala katika jiji la Dar es Salaam, nauli za usafiri wa reli ya kati na bandari.
Viwango hivyo vimetolewa kutokana na SUMATRA kufuatia maombi rasmi
kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri na makampuni binafsi nchini
kutokana ongezeko la gharama za uendeshaji.
Ahmad Kilima ni Kaimu
mkurugenzi mkuu wa SUMATRA amesema viwango vipya vimetolewa baada ya
kufuata taratibu za kisheria na utendaji kwa kuwashirikisha wadau
mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu ongezeko la nauli.
Amesema SUMATRA imeongeza viwango vya juu vya nauli ya daladala kwa
wastani wa asilimia 24.46 na mabasi ya masafa marefu viwango vimeongezwa
kwa asilimia 20.3
Pia amesema ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati
ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, mamlaka
imewataka wamiliki wa mabasi kutotumia wapiga debe katika kuuza tiketi
za usafiri na kwamba watakaokaidi hatua za kisheria zitachukuliwa.
Bwana Kilima amesema katika kufanya mapitio ya gharama mbalimbali za
bandari na bahari kuu mamlaka imeridhia ongezeko la gharama kwa
wastani wa asilimia 34.3 hivyo TPA wametakiwa kuboresha huduma kwa
wateja kwa kuanzisha kitengo cha huduma kwa wateja .
Hata hivyo
ongezeko hilo la nauli limeenda sanjari na viwango vya nauli kwa
usafiri wa abiria wa reli ya kati ambapo mamlaka imewataka abiria kukata
tiketi na kupanda treni wakionyesha vitambulisho…
Viwango vipya
vya nauli vinatarajia kuanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili 2013
ambapo nauli ya mwanafunzi itakuwa shilingi 200 na mtu mzima atalipa
shilingi 400 kwa safari za mijini.
Tuesday, April 2, 2013
Post a Comment