MWILI
WA ALIYETUHUMIWA KWA MAUAJI YA MTOTO AYUBU AGEN UKIWA UMECHOMWA MOTO
NAWANANCHI WENYE HASIRA KALI BAADA YA KUMKUTA MITA CHACHE KUTOKA KWENYE
MWILI WA MAREHEMU AKIWA NA KISU KINACHODHANIWA KUTUMIKA KATIKA MAUAJI
|
MWILI WA MTOTO AYUBU UKITOLEWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANAWILAYA YA RUNGWE |
SAFARI YA KUELEKEA KIJIJI CHA IJOKA KWA MAZISHI
-wananchi wapanda hasira wamteketeza kwa moto mtuhumiwa.
- ajali nazo zamaliza watatu sherehe za pasaka.
Na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
MATUKIO ya kutisha na
ya kinyama dhidi ya watoto wadogo yameendelea kuutikisa Mkoa wa Mbeya, baada ya
mwanafunzi wa chekechea, Ayoub Agen (6) kuuwa kwa kuchinjwa mithili ya kuku na
wauaji kuondoka na kichwa chake.
Hata hivyo wananchi
wenye hasira walifanikiwa kumnasa mmoja wa watuhumiwa wa tukio hilo, ambaye
hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana ambapo baada ya kummbana ili aeleze
sehemu walikokificha kichwa cha marehemu aligoma hivyo kuamua kumteketeza
kwa moto.
Habari za uhakika
kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Ijoka
katika kata ya Mpombo, wilayani Rungwe, Rafael Mwaikenda, zinadai kuwa
tukio hilo lilitokea Machi 31 majira ya saa 11:00 jioni.
Akifafanua zaidi
Mwenyekiti huyo alisema, marehemu Agen alikuwa ni mwanafunzi wa
chekechea katika shule ya msingi Lusanje kijijini hapo na kwamba alikutwa na
mauti hayo ya kikatili baada ya watu hao wasiofahamika kufanikiwa kumuiba
nyumbani kwao.
Mwaikenda
alisema mwili wa marehemu uliokotwa ukiwa umetenganishwa kichwa na
kiwiliwili huku kichwa kikiwa hakionekani hadi sasa ikiwa ni muda mfupi tu
baada ya watu hao wasiofahamika kumwiba toka nyumbani kwa wazazi wa marehemu .
“Marehemu
alichukuliwa na watu hao wasiofahamika akiwa anacheza na wenzake na wenzake
baada ya kuona hivyo waliamua kutoa taarifa ambapo muda mfupi walianza
kumtafuta bila mafanikio, lakini wananchi wakiwa wanaendelea na harakati hizo
waliukuta mwili huo ukiwa umetelekezwa kichakana na wauaji hao kuondoka na
kichwa” alifafanua Mwaikenda.
Mkazi mwingine katika
kijiji hicho, Tumpale Sankemwa, alikielezea mkasa huo, alisema baada ya
wananchi kugundua mwili huo wa marehemu waliendelea kuwasaka wahusika na wakiwa
katika harakati hizo ghafla walikutana na mtu mmoja ambaye walimtilia mashaka.
Alisema baada ya
kumfanyia mahojiano ya kina kwa kuwa alikuwa hafahamiki na mgeni kijijini hapo,
alikuwa akijibu jeuri hivyo kuwapandisha hasira wananchi jambo lililosababisha
kuanza kumshambulia na hatimaye kumuua papo hapo.
Hata hivyo alisema
wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigon mtu huyo licha ya kutotaja jina
lake, alikiri kuhusika katika tukio hilo kwa kueleza kuwa waliohusika walikuwa
watatu na kwamba wenzake walikuwa wameondoka.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi,Diwani Athumani,
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa kichwa cha marehemu
huyo hakijaonekana na jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi.
“Ni kweli tukio hilo
limetokea, hata hivyo mtu anayetuhumiwa kushiriki mauaji hayo naye aliuawa kwa
kupigwa na wananchi wenye hasira ambao licha ya kumuua waliuteketeza
mwili wake kwa moto”.
Aliongeza kuwa
mtuhumiwa wa mauaji hayo ni mwanaume anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 30
hadi 35 na kwamba uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha mauaji hayo
kinahusishwa na imani za kishirikina.
Wakati huo huo watu
watatu wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya,
katika matukio mawili tofauti ya ajili za barabarani mkoani hapa.
Katika tukio la
kwanza lililotokea eneo la Mbalizi wilayani hapa, majira ya saa nne usiku
katika barabara ya Mbeya- Tunduma, watu wawili, Meshaki Inkuru (24) na
Said Ndasi (19) baada ya gari aina ya Toyota Chesser yenye nambari za
usajili T 516 AAA lililokuwa likiendeshwa na mtu asiyefahamika kuwavamia
wakiwa nje ya Hoteli ya Royal Tughimbe walikokuwa wakiendelea na sherehe za
Pasaka.
Kamanda wa polisi
aliwataja majeruhi wa tukio hilo ambao wamelazwa katika Hospitali teuli ya
wilaya ya Mbeya ya Ifisi ni Shar Mkumbwa (20), Juliet Katemi (18)
wote wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi.
Tukio
lingine ni lile lililotokea eneo la Soweto ambapo mtu mmoja mtembea kwa
miguu, aliyetambuliwa kwa jina moja la Paul (60) kufa papo hapo baada ya
kugongwa na gari ambayo hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja |
Post a Comment