Loading...

Mkutano wa CHADEMA waruhusiwa Songea.Habari tulizozipata hivi punde zinasema Baada ya Mkutano wa pamoja kati ya viongozi wa vyama vya siasa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, hatimaye Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA kimeruhusiwa kufanya Mkutano wake wa kampeni ya M4C uliopangwa kufanyika tarehe 26 Mei 2013. Mkutano huo utafanyika Mjini Songea katika eneo la Matarawe Mjini Songea.

Hata hivyo katika makubaliano hayo, CHADEMA imekataliwa kufanya maandamano kama ilivyopangwa awali ambapo ilitangazwa kuwa Mkutano wa hadhara ungetanguliwa na maandamano ambayo yangeanzia katika Chuo Kikuu Huria hadi Matarawe.

Kufutwa na baadaye kuruhusiwa kwa Mkutano wa CHADEMA kumeleta mkanganyiko kwa wananchi wa Manispaa ya Songea kutokana na kubadilika kwa maamuzi ya Dola katika kipindi kifupi.

Habari pia zinaeleza kuwa Baada ya Mkutano wa CHADEMA hapo Mei 26, Chama Cha Mapinduzi CCM pia kitafanya mkutano wake hapa Songea Juni 02, 2013 ambapo Katibu Mkuu wa CCM Abdulahaman Kinana anatarajiwa kufanya Mkutano huo ikiwa ni sehemu ya ziara ya viongozi waandamizi wa Chama hicho nchi nzima. Mikutano hiyo ina lengo la kukagua uhai wa Chama pamoja na kutembelea na kuzungumza na mabalozi wa nyumba kumi, viongozi wa mashina ambayo ni uti wa mgongo wa Chama, matawi, kata, wilaya na mkoa.
 Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top