MWANAMKE mmoja mkazi wa maeneo ya Ruhuwiko katika Halmashauri ya
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Sophia amejifungua watoto watano.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani hapa, Mganga Mkuu
Mfawidhi wa Hospitali ya Songea, Dk. Benedict Ngaiza, alisema mwanamke
huyo alijifungua salama na watoto wake wanaendelea vizuri.
Dk. Ngaiza alisema wauguzi wa hospitali hiyo walimpa huduma nzuri
mwanamke huyo jambo lililosaidia kujifungua salama watoto hao licha ya
kufanyiwa upasuaji.
Aliongeza kuwa Sophia alijifungua watoto hao jana majira ya saa 4
asubuhi katika hospitali hiyo huku mtoto wa kwanza akiwa na uzito wa
gramu 730, wa pili 810, wa tatu 670, wa nne 820 na wa tano gramu 430.
Alifafanua kuwa kati ya watoto hao waliozaliwa, watatu ni wa kiume na
wawili ni wa kike na kudai kwamba tukio hilo ni la kwanza kutokea
katika hospitali hiyo ambapo uzao huo ni wa pili kwa mama huyo.
Alibanisha kuwa katika mzao wa kwanza wa mama huyo alijifungua mtoto mmoja
Post a Comment