Loading...

Mpiga debe Songea Stendi afa kwa kujinyonga


Mpiga debe wa kituo kikuu cha mabasi katika halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Solomon Hamisi (43) mkazi wa Mfaranyaki mjini Songea amekutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba za viatu juu ya kenchi ya nyumba alimo kuwa akiishi chumbani kwake

Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusidelit Msimeki zimesema kuwa tukio hilo lilitokea juni 5 mwaka huu majira ya 6:00 mchanahuko katika eneo la Mfaranyaki mjini Songea. 

Kamanda Msimeki alisema kuwa inadaiwa tukio hilo liligunduliwa na Helena Ndonde (37) ambaye ni mke wa Hamisi ambaye alikutwa akiwa ananing’inia kwenye kenchi ndani ya chumba alichokuwa analala yeye na mke wake

Alifafanua zaidi kuwa Helena aligundua kujiua kwa mume wake kwa kujinyonga kwa kutumia kamba za viatu kwa kujining’iniza kwenye kenchi ya nyumba hiyo ambapo baada ya kugundua tukio hilo alitoa taarifa kwa majirani na baadaye uongozi wa serikali ya mtaa ulipopata taarifa ulitoa taarifa kwenye kituo kikuu cha polisi cha mjini Songea

Alibainisha zaidi kuwa baada ya polisi kupata taarifa ya tukio hilo askari polisi wakiwa wameongozana na daktari walikwenda kwenye eneo la tukio hilo na kumkuta Hamisi akiwa amening’inia juu ya kenchi  ya nyumba na baada ya kumfanyia uchunguzi daktari alithibitisha kuwa Hamisi amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kamba za viatu

Hata hivyo kamanda Msimeki alisema kuwa chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa kwa kina zaidi ili kubaini sababu zilizomfnya Hamisi achukue uamuzi mgumu wa kujinyongaPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top