Loading...

ISPEKTA CHACHA AHIMIZA USAWA WA KIJINSI KWA MAENDELEO ENDELEVU

Na Stephano Mango, Songea

WANANCHI wametakiwa kuheshimu usawa wa kijinsia katika mchakato mzima wa kuleta mabadiliko ya kijamii ,kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni ili kuleta maendeleo endelevu katika jamii zetu kwa kuzingatia uangalifu wa kisheria

Wito huo umetolewa leo na makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoani Ruvuma Ispekta Fadhira Chacha wakati akitoa mada kwenye mdahalo wa wazi ya Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo uliofanyika Kata ya Magagura Jimbo la Peramiho, Wilaya ya Songea ulioitishwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Songea(Sonngo) kwa ufadhiri wa The Foundation For Civil Society

Ispekta Chacha alisema kuwa wanawake na wanaume ni mawakala wakuu wa maendeleo na sio wapokeaji wa maendeleo na mabadiliko ambayo yanaiwezesha jamii kuweza kupata mahitaji yake na kuboresha maisha kwa kuzingatia mgawanyo sawa wa rasilimali

Alisema kuwa ili kuleta maendeleo uchambuzi wa mahitaji ya wake kwa waume waweza kufanyika kwa uwepo majadiliano,kuthubutu,kutoa mrejesho,kulinganisha na kuchanganua ni vitu vipi vinavyotakiwa ili kuleta maendeleo sawa

Kwa upande wake Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo alieleza kwenye mdahalo huo kuwa vitendo vya ukatili vinavyoendelea kuathiri maisha ya watu wengi katika jamii zetu jambo ambalo husababisha madhara kimwili na kiakili

Ngarimanayo alisema kuwa ukatili wa kijinsia hudumaza maendeleo kwani waathirika hushindwa kufanya majukumu yao,kupoteza fedha,muda katika kutibu majeraha,ongezeko la walemavu na kutoweka kwa upendo

Awali akieleza maudhui ya mdahalo huo Mwenyekiti wa Sonngo Siwajibu Gama alisema kuwa lengo kubwa ni kuelimishana,kuhabarishana na kujengana uwezo wa kujiletea maendeleo kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, hivyo elimu hiyo inapaswa iwe mbegu ya kuleta mbegu ambayo itazaa matunda stahiki katika jamiiPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top