Loading...

Songea yaendelea kukumbwa na giza, tatizo ukosefu wa mafuta ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme

Na songeayetu.blogspot.com
MANISPAA ya mji wa Songea inaendelea kukumbwa na tatizo la umeme katika maeneo yake mengi kutokana na shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuishiwa mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo yake ya kufua umeme iliyopo maeneo ya Kiburang'oma. Kwa mfululizo siku tatu mji wa songea umekumbwa na giza kutokana na kukatwa kwa umeme.

Kaimu meneja wa Tanesco mkoa wa Ruvuma ndugu Haruna Mwachuya amethibitisha kuwepo kwa tatizo hilo ambalo limesababishwa na ukosefu wa mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo ambapo amebainisha kuwa kwa sasa shirika hilo huzalisha umeme kiasi cha mega watt 1.5 ambapo mahitaji kamili ya umeme kwa manispaa ya Songea na vitongoji vyake ni mega watt 4.5

Haruna amedai kuwa ili kuweza kuzalisha umeme kiasi cha kutosheleza mahitaji ya umeme kwa megawati 4.5 Tanesco inahitaji kiasi cha lita 20000 za mafuta kwa siku ambapo imeonekana kuwa ni gharama kubwa kwa uendeshaji wa mitambo hiyo. Pia kaimu meneja huyo amedai kuwa kwa sasa mashine zilizokuwa katika matengenezo tayari zimetengenezwa na iwapo kutakuwa na mafuta ya kutosha tatizo la umeme laweza kupungua katika mji wa Songea.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top