Loading...

WASAMALIA WAOMBWA KUTOA MSAADA WA MATIBABU KWA MTOTO FAHAHATI

Na Steven Augustino, Tunduru

WASAMALIA  nchini wameombwa kutoa msaada wa hali na mali ili kusaidia matibabu ya Mtoto Fahahati Rajab anayetakiwa kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa sehemu ya kutolea haja kubwa na matundu ya masikio.
Ombi hilo limetolewa na wazazi wa Mtoto huyo Bwana na Bibi Rajab Idd wakidai kuwa hali hiyo imetokana na familia yao kutokuwa na uwezo wa kughalamia matibabu hayo yanayotarajiwa kufanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Walisema Mtoto huyo aliyezaliwa akiwa hana sehemu ya kutolea haja kubwa na matundu katika masikio July 4 2011 katika Hospitali ya Missioni ya Mbesa Wilayani humo ambako  awali watalamu wake waliahidi kutoa msaada wa matibabu lakini kadili siku zilipo enda waliwajibu kuwa wameshindwa na kuwaomba wampeleke muhimbili.

Walisema mtoto huyo ambaye ni mzao wao wa kwanza kwa sasa ana umri wa miezi 11 hula na  hujisaidia kupitia mdomoni hali ambayo imekuwa ikiwawia vigumu watu wangine kumsaidia kutokana na kuona kinyaa.

Walisema kuwa atakaye guswa na hali hiyo anaombwa kutoa msaada wake autume kwa njia ya M-pesa kupitia namba  0758168501 inayo mirikiwa na Baba Mzazi wa Mtoto huyo  Rajab Idd ili kuwawezesha kusafiri hadi jijini Dar es Salaam na kughalimia matibabu hayo.

Akizungumzia tukio hilo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Serikali ya Wilaya Tunduru Dkt.Alex Kazula alisema kuwa hospitali yake ina andaa utaratibu wa kumpeleka Mtoto huyo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.
Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top