Na Stephano Mango, Nyasa
MKUU wa wilaya ya nyasa Mkoani Ruvuma Ernest Kahindi amesema kuwa kauli mbio yake katika kuhimiza maendeleo wilayani humo ni amani na maendeleo ambayo inahimizwa kwa wakazi wote wa wilaya hiyo wenye uwezo wa kufanya kazi na amewatahadharisha wananchi kutokunywa pombe wakati wa saa za mchana na badala yake waone umuhimu wa kufanya kazi mbalimbali zitakazoweza kuwaletea kipato.
Kahindi aliyasema hayo jana kwenye mji mdogo wa Mbambabey ambapo alifafanua kuwa amani ni kupambana na mambo mbalimbali ya uharifu mfano ujambazi,uhamiaji haramu ,unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji ,rushwa ,mimba kwa watoto wa shule za msingi na sekondari .
Alisema kuwa maendeleo kila mkazi mwenye uwezo wa kufanya kazi ni lazima awajibike kikamilifu ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wakazi wote wa wilaya mpya ya nyasa kwa kuelekeza nguvu kwa kuhakikisha wananchi wanaondokana na ujinga, maradhi na umasikini.
Aliendelea kufafanua kuwa ujinga ndio unahathari kubwa hivyo mtazamo wake utakuwa ni kusimamia swala zima la Elimu hasa ikizingatiwa kuwa kila kata kuna shule za msingi na sekondari hivyo watoto wenye umri wa kwenda wa kuanza kwenda shule ni lazima wazazi wao wawapeleke kwenye shule ili kuondokana na tatizo sugu la ujinga na wanafunzi ambao wanaonekana kuwa ni watoro kwenye shule za sekondari za kata wajirudihe wenyewe badala ya kufuatwa na mkono wa dola na si vinginevyo.
Alieleza zaidi kuwa amewaagiza maafiza watendaji wa kata zote kuhakikisha kuwa wanawasiliana na wakuu wa shule za sekondari za kata ili kuwabaini wanafunzi watoro ambao wanapaswa warejee kwenye shule zao kabla ya hatua zingine kuanza kuchukuliwa.
Amewaonya baadhi ya wavuvi katika ziwa nyasa wenye tabia ya kuwatumia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwenye shughuri zao za uvuvi na badala yake wawahimize wanafunzi hao kwenda shuleni na kwamba mvuvi yeyote katika wilaya ya nyasa anawaajili wanafunzi kazi ya kuvua samaki kwenye ziwea nyasa atachukuliwa hatua za kisheria mara moja..
Alisema kuwa wilaya ya nyasa wananchi wake ni wakulima na wavuvi wa samaki hivyo kazi kubwa mbele yake ni kuhakikisha kuwa wilaya hiyo inakuwa na mazao ya chakula na biashara ambapo aliyataja mazao ya chakula kuwa ni mahindi, muhogo na mpunga na mazao ya biashara ni kahawa na korosho.
Alibainisha zaidi kuwa vijana wote katika wilaya hiyo wenye uwezo ni lazima wafanye kazi bila kuchagua kazi na waachane na swala la kunywa pombe nyakati za saa za mchana na badala yake waone umuhimu wa kubuni miradi mbalimbali za maendeleo zitakazo weza kuwakwamua kiuchumi.
Aidha amewahimiza wawekezaji hapa nchini kuona umuhimu wa kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa kandokando ya ziwa nyasa ambako kuna vivutio vingi vya utalii kwa kuweka mahoteli, viwanda na taasisi za fedha (bank ) hasa katika miji midogo ya Litui,Lihuli na mbambabey ambako ndio makao makuu ya wilaya hiyo.
Post a Comment