Loading...

Lori lauwa Songea


CHARLERS Dominick (34) maarufu kwa jina la Mgaya mkazi wa eneo la mjimwema katika halmashauri ya manispaa ya Songea amekufa papo hapo baada ya gari alilokuwa akiendesha kuacha njia na kugonga daraja kasha kutumbukia mtoni.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedilit Msimeki alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 6:30 mchana huko katika kijiji cha Lilpokela kilichopo wilaya ya Songea vijijini kwenye barabara ya kutoka Songea mjini kwenda Mbinga.

Kamanda Msimeki alisema kuwa gari hiyo aina ya Shacmam lori ambalo ni mali ya kampuni ya ujenzi wa barabara kwa  kiwango cha lami kutoka Songea kwenda Mbinga ya Synohydro ya China ambalo lilikuwa likitokea eneo ya njia panda ya Peramiho kwenda Lipokela kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa barabara hiyo.
Alifafanua zaidi kuwa gari hiyo ambayo ilikuwa haina namba za usajiliyenye chesesi namba L2GJBR61.BX078061 ikiwa kwenye mwendo mkali iliacha njia na kugonga kingo za daraja na baadaye ilitumbukia kwenye mto Ruvuma na kusababisha dereva wa gari hiyo kufa papo hapo.

Hata hivyo kamanda Msimeki alieleza zaidi kuwa inadaiwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo mkali lakini  jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kufanya upelelezi zaidi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top