Loading...

WAWILI WAFA NA WENGINE 355 WAJERUHIWA BAADA YA KUNG’ATWA NA MBWA WANAODAIWA KUWA NA UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA



WATU wawili walifariki dunia  na  wengine  355 walilipotiwa kung’atwa na mbwa katika kipindi cha januari hadi juni mwaka huu Mkoani Ruvuma ambapo wananchi wameshauriwa kuwa waangalifu na mbwa wanao zulula hovyo mitaani .

Hayo yalisemwa jana na afisa wa afya katika ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Sabina Nyamuka wakati alipokuwa akiongea na NIPASHE ofisini kwake.

Afisa wa afya Nyamuka alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia januari hadi juni mwaka huu kulikuwa na taarifa ya vifo vya watu wawili tofauti na kipindi cha mwaka jana ambacho kilikuwa na taarifa ya kifo kimoja na watu 779 walilipotiwa kung’atwa na mbwa .

Alieleza zaidi kuwa Mkoa wa Ruvuma ambao unawilaya za Mbinga,Tunduru, Songea ,Namtumbo na Nyasa  tayari kuna hatua zinachukuliwa za kuhakikisha kuwa dawa za chanjo zinakuwepo za ugonjwa huo wa kichaa cha mbwa zinakuwepo kwenye Hospitali zote za serikali za wilaya.

Alifafanua zaidi kuwa hatua nyingine iliyochukuliwa ni kutoa elimu kwa jamii katika ngazi zote za vikao ya Halmashauri za wilaya na Manispaa pamoja na kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma za afya kwa kuwaelimisha kwa makini zaidi wagonjwa na kuwahi kupata tiba na kinga pale wanapong’atwa na mbwa wanaosadikiwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

Alifafanua kuwa tangu januari hadi juni mwaka huu watu wawili walifariki dunia katika maeneo ya mateka na Liwena yaliyopo kwenye Halmashauri ya manispaa ya Songea na kwamba idadi kubwa ya watu waling’atwa na mbwa ni kutoka wilaya ya mbinga .

Alisema kwa upande wa sekta ya idara ya mifugo Mkoani humo amewahimiza maafisa mifugo wa  ngazi zote kuona umuhimu zaidi wa kotoa chanjo kwa mbwa na pia kuwauwa mbwa wanaoonekana kuzulula hovyo mitaani ambao wanaweza kusababisha zaidi ugonjwa huo ambao ni hatari.

Nyamuka alisema kuwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa unasababishwa na kuumwa na mbwa pamoja nawanyama wa polini wanao sadikiwa kuwa na Virusi  vya ugonjwa wa kichaa cha mbwa ambapo aliwataja baadhi ya wanyama ambao ni hatari kwa ugonjwa huo kuwa ni Mbwa,Mbweha na Nyani.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top