Loading...

Mwendesha pikipiki afa kwa kuangukia uvunguni mwa gari


MWENDESHA pikipiki Erasto Hyera (35) mkazi wa kijiji cha Unyoni wilayani Mbinga mkoani Ruvuma amekufa papohapo baada ya pikipiki aliyokuwa akiiendesha kugongana na pikipiki nyingine ambaye namba zake za usajili hazikuweza kufahamika mara moja .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Deusdedit Msimeki alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 3 mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni kwenye eneo la gurio la kijiji cha Unyoni  kwenye barabara itokayo unyoni kwenda kijiji cha Maguu.

Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio pikipiki yenye namba za usajili T 336 BUH aina ya SANLG iliyokuwa ikiendeshwa na Hyera iligongana na pikipiki nyingine ambayo namba zake za usajili hazikuweza kuonekana mara moja kwani mwendesha pikipiki hiyo baada ya kusababisha ajali hiyo alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Alifafanua kuwa inadaiwa Hyera alikuwa akiendesha pikipiki akitokea katika kijiji cha unyoni kwenda katika kijiji cha Maguu na alipofika kwenye eneo la gurio akiwa anajaribu kutaka kuipita pikipiki iliyokuwa mbele yake ghafla aliigonga na baadaye alisababisha pikipiki yake kuangukia  uvunguni mwa gari lenye namba za usajili T 528 ALG aina ya Isuzu Escudo na kumsababishia kifo chake papo hapo.

Alisema kuwa gari hiyo ambayo ilikuwa ikitokea Unyoni kwenda Mbinga ambayo dereva wake baada ya kugundua ajali hiyo alikimbia na kuicha gari yake eneo la tukio na baadaye alirudi na kujisalimisha kwenye uongozi wa serikali ya kijiji hicho na kwa sasa anaendelea kuhojiwa zaidi na jeshi la polisi licha ya kuwa mazingira ya ajali hiyo mwendesha aliangukia kwenye uvungu wa gari lake.

Hata hivyo kamanda Msimeki alisema kuwa jeshi lake la polisi mkoani humo linaendelea kufanya uchuzi zaidi kuhusiana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kumsaka mwendesha pikipiki ambaye alikuwa akiendesha pikipiki iliyosababisha ajali ambaye jina lake pamoja na namba za usajili za pikipiki yake hazikuweza kufahamika mara moja baada ya kukimbia na kutokomea kusikojulikana baada ya ajali hiyo kutokea.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top