Loading...

Ruvuma: Mwanamke afa kwa kunywa Sumu


MWANAMKE mmoja Isdora Nchimbi (30) mkazi wa kijiji cha Manzege kilichopo katika kata ya Ngima wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma amefariki baada ya kunywa sumu  ya kuulia wadudu kwenye mashamba ya kahawa.

Habari zilizopatikana jana mjini Mbinga ambazo zimethibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Deusdediti Msimeki zilisema kuwa tukio hilo lilitokea julai 3 mwaka huu majira ya saa 7 mchana huko katika kijiji cha Manzege.

Kamanda Msimeki alifafanua zaidi kuwa inadaiwa kuwa mwanamke huyo Isdora akiwa nyumbani kwake siku ya tukio alikunywa sumu ya kuulia wadudu kwenye mashamba ya kahawa aina ya Round up.
Alisema kuwa mwanamke huyo Isdora baada ya kunywa sumu watu waliokuwa jirani walipomwona walimchukua na kumkimbiza katika hospitali ya misheni ya Litembo inayomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la Mbinga.

Alibainisha zaidi kuwa isdora akiwa hospitali huku akiendele kupata matibabu ilipofika mida ya saa 10:30 jioni alifariki dunia na kwamba inadaiwa kuwa chanzo inasadikiwa kuwa ni ugomvi wa kifamilia ambao ulianza kati yake na mume wake Flavian Komba (32) ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top