Loading...

wawili wapandishwa kizimbani kwa makosa mawili tofauti mjini Songea

DEUSDEDITY Mtala (34) mkazi wa kijiji cha Peramiho kilichopo katika wilaya ya Songea amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Ruvuma kujibu shitaka la kukutwa akiwa anamiliki siraha bila ya kuwa na kibali.

Mwendesha mashtaka wakili wa serikali kanda ya Songea  Hamimu Nkoleye mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Ruvuma Kasmilly Mwalunyungu alisema kuwa mshtakiwa Ntala anashtakiwa kuwa mnamo julai 16 mwaka huu majira ya saa za mchana huko katika eneo la kijiji cha Peramiho wilaya ya Songea bila halali alikamatwa akiwa anamiliki bunduki aina ya shortgun.

Mshitakiwa Ntala baada ya kusomewa shitaka hilo alikana shitaka na alipelekwa rumande hadi agosti mwaka huu kesi yake itakapo tajwa tena.

WAKATI HUO HUO katika mahakama hiyo Timotheo Mboya (19) mkazi wa kata ya Mfaranyaki katika halmashauri ya manispaa ya Songea amefikishwa mahakamani kujibu shitaka la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka kumi na sita amnbaye jina lake limehifadhiwa.

Mwendesha mashtaka wakili wa serikali kanda ya Songea Hamim Nkoleye mbele ya hakimu mkazi wa mahakama wa mkoa wa Ruvuma Kasmilly Mwalunyungu alidai kuwa Mboya anashtakiwa kuwa mnamo machi 20 mwaka jana huko katika eneo la kata ya Mfaranyaki  alitenda kosa la kumbaka msichana (16) bila ridhaa yake na kumsababishia maumivu makali.

Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka na amepelekwa rumande hadi agosti 3 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top