Loading...

Ahukumiwa jela miaka 20 kwa kutaka kubaka mtoto wa miaka minne mjini Songea

Na Gideon  Mwakanosya, Songea

MAHAKAMA ya hakimu mkazi mfawidhi mkoani Ruvuma imemhukumu Rashid Hussein (46) maarufu kwa jina la Nangwele mkazi wa eneo la Majengo manispaa ya Songea kwenda jela miaka ishirini baada ya kupatikana na hatia ya shambulio la aibu la kutaka kujaribu kumbaka  msichana mwenye umri wa miaka minne ambaye jina lake limehifadhiwa.

Akisoma hukumu hiyo jana mahakamani hakimu mkazi mfawidhi wa  mahakama ya mkoa wa Ruvuma Frank Mahimbali alisema kuwa kutokana na ushahidi wa upande wa mashtaka uliotolewa mahakamni hapo na watu wanne tofauti  akiwemo mhanga umebainisha wazi kuwa mshtakiwa alikutwa akiwa anatenda kosa ambalo ni la shambulio la aibu.

Hakimu Mahimbali alifafanua zaidi mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Hussein ushahidi umeonyesha wazi kuwa alikutwa akiwa amevua nguo zake na uume wake ukiwa umesimama huku akiwa amemshika msichana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa ambaye pia nguo zake zilikuwa zimevuliwa huku akiwa anachezea uume wake kwenye sehemu za siri za msichana huyo.

Alisema kuwa mahakama baada ya kutafakari na kutathmini ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa mashtaka mahakama  imebauini kuwa kosa alilotenda mshitakiwa lililothibitishwa mahakamani kwa ushahidi uliotolewa ni la shambulio la aibu dhidi ya msichana huyo ambalo ni kosa chini ya kifungu 138C kifungu kidogo cha kwanza hivyo mshitakiwa anahukumuiwa kutumikia adhabu ya kifungo jela miaka ishirini sambamba na kulipa fidia ya jumla ya shilingi liki tano kwa mwathirika.

Hata hivyo mshitakiwa Hussein baada ya kutiwa hatiani alipewa nafasi na mahama ya kujitetea ambapo aliiomba mahakama iangalie namna ya kumhurumia hasa ikizingatiwa kuwa ana familia inayomtegemea, kwa upande wake mwendesha mashtaka wakili wa serikali Mwegora aliiomba mahakama iangalie uwezekano wa kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili liwe fundisho kwa wengine

Awali mwendesha mashtaka wakili wa serikali Shaban Mwegora mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Ruvuma Francis Mahimbali ulidai kuwa mnamo januari 26 mwaka huu majira ya saa za mchana huko katika maeneo ya Majengo Rashid Hussein maarufu kwa jina la Nangwele katika hali isiyo ya kawaida alikutwa akitaka kujaribu kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne ambaye jina lake limehifadhiwa tukio ambalo ni la aibu.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top