Loading...

ASAKWA KWA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO NA KUCHANA RAMANI YA SENSA

Na Agustino Chindiye, Tunduru MKAZI wa Kijiji cha Nampungu wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma aliyefahamika kwa jina la Said Mkepa anatafutwa na Jeshila Polisi kwa tuhuma za kufanya fujo na kuchana Ramani iliyotakiwa kutumika na karani wa kuandikisha wananchi katika Zoezi la kuhesabu watu katika Sensa ya Watu na makazi inayoendelea nchini kote.

Msako huo umefuatia agizo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Chande Nalicho kwa jeshi hilo na akaongeza kuwa kitendo hicho kilichofanywa na mwanachi huyo pamoja na makundi mengine hakiwezi kuvumiliwa. Akifafanua taarifa hiyo alipotakiwa kuzungumzia maendeleo ya zoezi hilo katika Wilaya yake pamoja na kutaja changamoto mbalimbali zilizojitokeza siku ya kwanza Dc, Nalicho alisema kuwa mbali na kuwepo kwa changamoto hizo Wananchi wengi walijiwekeza kuhesabiwa.

Aidha katika taarifa hiyo Nalicho alibainisha kuwa awali kulikuwa na vitendo vya waandikishaji kugomea zoezi hilo kwa nia ya kushinikiza malipo yao tatizo ambalo lilitatuliwa baada ya mtandao wa Benki ya NMB tawi la Tunduru kuanza kufanya kazi na kufanya fedha zao kupatikana na kulipwa usiku wa kuamkia Agosti 26, mwaka huu.

Nalicho aliendelea kufafanua kwa kuyataja matukio mengine yaliyo onekana kuwa kikwazo cha kufanikisha zoezi hilo kuwa ni mgomo wa kuhesabiwa kwa wauzaji wa mnada lililotokea katika kijiji cha Ligunga na Waislam wa Taasisi ya Tabrig ambao walijifungia katika msikiti wa kijiji cha Kajima katika Kata ya Kalulu matukio ambayo alisema kuwa yanaendelea kutafutiwa ufumbuzi na kuhakikisha kuwa wanahesabiwa.

Akizungumzia suala la waumini wa madhehebu hayo Nalicho alisema kuwa tayari kuna taratibu za kuwasiliana na viongozi wa madhehebu hayo zinaendelea ili kutatua mgogoro huo ambapo waumini hao katika maelezo yao wanadai kuwa wao wamehesabiwa kupitia wake zao waliopo Jijini Dar es salaam na kwamba endapo wataendelea kugoma serikali itazuia vibali vyao vya kuendelea kueneza dini Wilayani humo pamoja na kuchukua hatua za kisheria.

Nae Mratibu wa Sensa Wilayani humo Rudrick Charles katika taarifa yake alisema kuwa kwa ujumla zoezi hilo linaendelea vizuri ukioondoa vikundi vidogo vidogo vikiwemo kikundi cha wauzaji mnada waliogomea zoezi hilo katika kijiji cha Lingunga na waislam wa Taassisi ya Tarig ambao alidai kuwa tayari ofisi yake imekwisha patiwa majina ya watu wote na kwamba utaratibu wa kuwakamata unafanyika na kuangalia hatua za kuwachukulia endapo wataendelea kugoma kuhesabiwa.


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top