Na Giden Mwakanosya, Songea ALIYEKUWA Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mjimwema iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoa wa Ruvuma Magdalena Zuru Gama amejivua uwanachama wa chama hicho na amejiunga katika Chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) na amedai kuwa amefanya uamuzi huo akiwa na akili timamu ambapo ameeleza kuwa ameona chama hicho kinaendelea kukosa maendeleo na baadhi ya viongozi wa mejaa ubinafsi. Magdalena Gama alitoa kauli hiyo jana kwenye ofisi ya chadema kata ya Mjimwema wakati alipokuwa akikabidhiwa kadi mpya ya CHADEMA baada yakuomba na chama hicho kwa mwenyekiti wa CHADEMA wa tawi la Pachanne lililopo Mjimwema Swedi Milanzi ambako kulihudhuliwa na wanachama wa chama hicho. Alisema kuwa ameamua kukihama chama cha CCM baada ya kuona baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa na tabia ya ubinafsi na kuonekana kuwa CCM ni ya kwao wao wenyewe na kwamba kila nafasi inayotangazwa kugombea wanafanya kila njia wagombee wao wenyewe na kuwakatisha tamaa wanachama wengine wanaotaka kugombea nafsi hizo. Alifafanua zaidi kuwa alijiunga na uwananchama wa CCM tangu mwaka 1981 baada ya kupata mafunzo ya elimu ya siasa kwa muda wa miezi 3 hivyo alikuwa mwanachama wa muda mrefu na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za chama hicho licha ya kuwepo mizengwe ya hapa na pale iliyokuwapo ikifanywa na baadhi ya viongozi ambao walioifanya chama cha CCM ni mali yao,hivyo ameamua kujiunga na chama cha Chadema ambacho ndio chama pekee chenye sera nzuri zenye tija kwa watanzania. Kwa upande wake mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya chama hicho Samweli Chale alisema kuwa kitendo alichokifanya Magdalena Gama kukihama chama cha Ccm na kukimbilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni cha kiungwana kwani Ccm imejaa fitina hasa kwa wale Viongozi wanaoonekana kwa jamii kuwa makini. Chale ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha Democrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Bombambili alisema kuwa msimamo wa Chadema ni kuboresha zaidi maendeleo mbalimbali ya wananchi na kila malengo makini ya kuhakikisha kuwa chama kinashika dola kuanzia ngazi ya uongozi wa Serikali za mitaa,vitongoji na vijiji na kwamba hakuna chama kingine chenye kipaombele ni Chadema peke. Naye Mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema(Bavicha) wa Kata ya Mjimwema John Mkina alieleza kuwa nguvu ya chama inazidi kuongezeka na alidai kuwa baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wameonesha nia ya kutaka kujiunga na chama hicho hivyo Magdalena Gama ni sehemu ya wananchama wengi waliomba kutaka kujiunga na Chadema ambao wanataraijwa kukaribishwa kwa mikono miwili kujiunga na chama hicho
Loading...
Post a Comment