Loading...

MHASIBU WA RAS RUVUMA ATIWA MBARONI KWA KUMPIGA RISASI MFANYAKAZI WAKE


Na Gideon Mwakanosya, Songea
MHASIBU wa ofisi ya katibu tawala mkoa wa Ruvuma anayeitwa Philemon Bosse (36) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumpiga risasi mfanyakazi wake anayeitwa Christopher Nyoni (27) mkazi wa Mateka katika halmashauri ya manispaa ya Songea.
Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa na ndugu wa karibu wa Nyoni ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe zimeeleza kuwa inadaiwa tukio hilo lilitokea septemba 16 mwaka huu majira ya saa nne usiku huko katika eneo la majengo karibu na Friends Grocery ambayo ni maarufu kwa kuuza vinywaji zikiwemo pombe za kigeni.
Alisema kuwa inadaiwa kuwa Nyoni alikutwa na mkasa huo baada ya kupigiwa simu na mwajili wake ambaye alimtaka aonane siku hiyo kwani kabla yake Nyoni alipewa ruhusa ya kwenda kijiji cha Luanda wilayani Mbinga ambako ndiko nyumbani kwao kuwaona ndugu.
Alifafanua zaidi kuwa septemba 12 mwaka huu, Nyoni alimwomba ruhusa bosi wake ambaye ni mwajili kake ili aende nyumbani kwao akawasilimie ndugu zake na septemba 15 mwaka huu inadaiwa bosi wake alimpigia simu Nyoni akimtaka alejee haraka Songea mjini ili aendelee na shughuli zake za kila siku.
Alisema kuwa hata hivyo inadaiwa kuwa Nyoni anadaiwa na mwajili wake kuwa amepoteza baadhi ya mali pamoja na fedha alizokuwa amekabidhiwa jambo ambalo linahofiwa kuwa ndiyo iliyosababisha bosi wake huyo kumjeruhi kwa kumpiga risasi Nyoni kwenye mkono wake wa kulia karibu na bega.
Alibainisha kuwa Nyoni baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi alikwenda kwenye kituo kikuu cha polisi cha Songea kutoa taarifa juu ya kujeruhiwa kwake kwa kupigwa risasi na mwajili wake kasha alipewa hati ya matibabu (PF 3) na baadae alielekea kwenye hospitali ya mkoa ambako alitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Kwa upande wake kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Msimeki alipohojiwa na NIPASHE jana ofisini kwake kuhusiana na tukio hilo alithibitisha kuwa septemba 16 mwaka huu majira ya 5.30 usiku katika kitiuo kikuu cha polisi cha Songea zilipokelewa taarifa kutoka Christopher Nyoni mkazi wa mateka kuwa amejeruhiwa kwa kupigwa risasi kwenye wake wa kulia karibu na bega akiwa eneo la majengo eneo mnadani.
Kamanda Msimeki alimtaja mtuhumiwa kuwa ni Philimon Bosse ambaye ni mhasibu katika ofisi ya katibu tawala mkoa wa Ruvuma ambapo alidai kuwa anatuhumiwa kumpiga mfanyakazi wake ambaye anajishughulisha na biashara ya kuuza nyama kwenye grocery yake iliyopo maeneo ya mateka na tayari mtuhumiwa amekwisha kamatwa na upelelezi kuhusiana na tukio hilo unaendelea kufanyika na kwamba ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
Mwisho

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top