Loading...

Kituo cha Afya Mjimwema Songea chakumbwa na uhaba wa madawa

Na Gideon Mwakanosya, Songea BAADHI ya wagonjwa wanaopata matibabu katika kituo cha afya Mjimwema kilichopo katika halmashauri ya manispaa ya Songea mkoa wa Ruvuma wamelalamikia kuwepo uhaba mkubwa wa madawa katika kituo hicho ambao unasababisha waganga kuwashauri wagonjwa kwenda kununua dawa kwenye maduma ya watu binafsi ambako wamedai kuwa daa hizo zimekuwa zikiuzwa kwa bei kubwa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wagonjwa hao ambao waliomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakifika kituoni hapo kwa lengo la kutaka kupata matibabu lakini badala yake zaidi wamekuwa wakipewa ushauri wa waganga na kuandikiwa dawa ambazo kwenye kwenye kituo hicho cha afya hazipo. Mmoja wa wagonjwa hao aliiambia NIPASHE kuwa yeye kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na kidonda lakini kila anapokwenda kwenye kituo hicho kwa ajili ya kusafisha amekuwa akishauriwa na waganga kuwa ni vyema aende akanunue dawa ya kusafishia vidonda kwenye maduka ya watu binafsi kwani kituo hicho kina tatizo kubwa la uhaba wa madawa kwa muda mrefu. Mgonjwa mwingine alipohojiwa akiwa kwenye eneo la kituo hicho alisema kuwa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria lakini kila anapofika kwenye kituo hicho anaambiwa hakuna dawa a badala yake anaelezwa kuwa aende kununua dawa alizoandikiwa na mganga kwenye maduka. Alisema kuwa jambo la kushangaza hata dawa za kutuliza maumivu (Panado) nazo wanadai kuwa hawana hivyo ameiomba serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii kuona umuhimu wa kuihimiza bodi ya madawa (MSD) kuhakikisha kuwa inasambaza madawa kwenye zahanati na vituo vya afya kwa wakati mwafaka ili kuokoa maisha ya watanzania ambao wengi wao wanaishi maeneo ya vijijini. Kwa upande wake mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mjimwema dkt. Daniel Mtamakaya alipohojiwa na NIPASHE kuhusiana na malalamiko ya wagonjwa juu ya uhaba wa madawa kwenye kituo chake alikili kuwa kwa muda mrefu kituo chake cha afya cha Mjimwema hakijapokea madawa toka bohari ya madawa MSD jambo ambalo amedai kuwa limekuwa likileta usumbufu mkubwa kwa wagonjwa ambao wamekuwa wakifika kituoni hapo ili kupata matibabu. Dkt Mtamakaya alisema kuwa kituo chake cha Mjimwema kimekuwa kikipokea wagonjwa wengi wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa malaria ambao umeonekana kuwa ni tishio kubwa kwa wakazi wa songea na kwamba kutokana na kuwepo kwa uhaba wa madawa wamekuwa wakilazimika kuwapa ushauri wa kitaalam lakini dawa ni lazima waende wakanunue kwenye maduka ya watu binafsi kwani tangu juni mwaka huu tatizo hilo la uhaba wa dawa limekuwepo na mpaka sasa ufumbuzi wake bado haujulikani. Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Songea Nachoa Zacharia ameiambia NIPASHE kuwa kuna tatizo kubwa la uhaba wa madawa kwenye zahanati zote za manispaa hiyo pamoja na kituo cha afya cha Mjimwema na kwamba Alisha watuma wataalam zaidi ya mara mbili kwenda kwenye bahari ya dawa kanda ya Iringa lakini wamekuwa wakilrudi mikono tupu wakidai kuwa MSD imesema kuwa haina madawa na kulazimika halmashauri ya manispaa ya Songea kutafuta njia nyingine ya kunuua madawa kwenye maduka ya watu binafsi na kuyapeleka kwenye zahanati na vituo vya afya jambo ambalo amedai kuwa ni gumu sana kwani dawa hizo zimekuwa zikinunuliwa kwa bei kubwa sana. MWISHO.


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top