Loading...

R.I.P Hussein Mkiety a.k.a Sharo Millionea!

MSANII WA VICHEKESHO NA MUZUKI SHARO MILIONEA  AMEFARIKI LEO HUKO MUHEZA TANGA KWA AJALI YA GARI AMBAPO NDUGU ZAKE WA KARIBU WAMETHIBITISHA TUKIO HILO 

 

Halikadhalika, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesikika akisema "majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”

Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sasa.
Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top