Loading...

SERIKALI YAADHIMIA KUONGEZA ADHABU KWA MAJANGILI

WAZIRI wa Mariasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki ameadhimia
kupeleka Bungeni maadhimio ya kubadilisha Sheria ili kuongeza adhabu
kwa watuhumiwa wa makosa ya Jinai za uhujumu uchumi ambavyo vimekuwa
vikifavywa na wawindaji haramu.

Hali hiyo imefuatia Serikali kubaini kushamiri kwa vitendo vya uhalifu
wa ujangiri kufuatia Oparesheni maalumu iliyofanyika Wilayani Tunduru
Mkoani Ruvuma na kufanikiwa kukamata mali zenyedhe dhamani ya Milioni
618.408

Akifafanua taarifa hiyo Waziri Kagasheki alisema kuwa kuanzi sasa
serikali haitawavumilia na kuwaacha wajanja wachache wakiendelea
kujinufaisha kupitia maliasiri za taifa hili huku kukiwa nakundi kubwa
wakibakia kuwa watazamaji huku akipendekeza kuwa adhabu za watuhumiwa
hao ziwe kati ya miaka 40 na 50.

Aidha pamoja na kuwapongeza askari waliofanikisha kukamatwa kwa mali
hizo Waziri Kagasheki alisema kuwa Oparesheni hizo ni endelevu na
akatumia nafasi hiyo kuwaomba Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano
utakaofanikisha kukamatwa kwa wahusika wengine waliokimbia.


Kwa mujibu wa taarifa za Oparesheni hiyo miongonimwa mali zingine
zilizo kamatwa katika Oparesheni hiyo ni pamoja na Bunduki zaidi ya
300 na Risasi 667 na Maganda ya Risasi 150 zilizobainika kumirikiwa
kinyume cha taratibu.

Mali zingine zilizokamatwa katika Oparesheni hiyo iliyo anza Oktober
20 mwaka huu ni pamoja na Gari moja aina ya Toyta, Piki piki 4 ambavyo
wahusika walivitelekeza na kuvikimbia baada ya kubainika kuwa vilikuwa
vimehusika kubeba Nyala za serikali.

Adha katika msako huo pia Mbao 10,183 zenye dhamani ya Shilingi
Milioni 377,257,000 zilikamatwa huku ailimia 90% ya Mbao hizo ni za
mti aina ya Mninga ambao namba 1A katika Soko la Dunia.

Akisoma Taarifa ya Oparesheni hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa
Oparesheni hiyo Bw. Samson Mkasla, Mtendaji wa Oparesheni hiyo
Bw.Emmanuel Kandihabi alisema kuwepo kwa mafanikio makubwa kutokana
ushiriliano mzuri kuitoka kwa Viongozi wa Serikali na waanchi wa
Wilaya hiyo.

Bw. Kandihabi aliendelea kueleza kuwa tayali Slaha zote zitahifadhiwa
Polisi katika kipindi cha Miaka Miwili na kwamba Wamiriki hao pia
ambao wamefungwa kifungo cha nje kwa muda wa Miaka miwili watatakiwa
kuomba upya baada ya muda huo kwisha.

Akizungumzia taarifa za matukio hayo Bw.Kandiahabi alisema kuwa
katika kipindi hicho walifanikiwa kukamata jumla ya waharifu 163
wakiwa na vilelezo vya Bunduki,Risasi,Meno ya tembo na Viboko,Mikia na
Singa za Tembo vyote vikiwa na thamani ya Shilingi 2,241,147 /22.

Alisema katika kipindi hicho pia Majalada 123 yalifunguliwa katika
Kituo cha Polisi Tunduru na tayari kesi 55 zimekwisha pelekwa
Mahakamani ambapo kesi 43 zimekwisha tolewa hukumukwa wahusika
kufungwa kati ya kifungo cha miaka 10 na miaka 5 jela huku wengine
wakitozwa faini.

Awali akisoma taarifa ya Wilaya hiyo kwa niaba Mkuu wa Wilaya ya
Tunduru Bw. Cande Nalicho Kaimu afisa Tawala wa Wilaya Bw. Manufred
Hyera alisema kuwa katika kuidhamini maendeleo ya idara hiyo tayali
Wilaya hiyo imetenga kiasi cha Shilingi 38,875,097/71  na Halmashauri
ya Wilaya hiyo  kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maliasili katika
kipindi cha mwaka 2012/2013.

Kikosi hicho kinacho shirikisha maafisa kutoka katika Majeshi ya
Polisi, Jeshi la wananchi,Usalama wa Taifa, Pccb,Magereza la
kuwashirikisha maafisa kutoka mamlaka ya Mapato TRA kinaongozwa na
Kamanda Mstaafu wa Jeshi la Polisi Bw. Venance Tosi.

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia hotuba Iliyotolewa na
Kamanda Tossi alisema kuwa oparesheni hiyo ni ya pili kufanyika na
kueleza kuwa oparesheni kama hiyo ilifanyika mwezi Julai katika
Wilayaya Liwale Mkoani Lindi.

MwishoPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top