Loading...

AJALI YATOKEA MLIMA KITONGA YAKWAMISHA ABIRIA KWA SAA 3

 

Magari mawili yamepata ajali jana katikati ya mlima Kitonga. Chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba T 722 ACJ lililobeba vifaa vya ujenzi lililindwa shindwa kuupanda mlima huo na kuanza kurudi nyuma. wakati linarudi nyuma kulikuwa na gari aina ya Toyota Corolla yenye namba T 138 ART ikitokea Kilombero kwenda Iringa iliyobeba watu wanne ikiendeshwa na dereva aliyejitambulisha kwa jina moja la Omary ikiwa kwenye mwendo kasi ilimbidi dereva wa gari hilo (Toyota) kutumbukiza gari hilo kwenye bonde kubwa la mlima huo umbali wa kama mita 45 kutoka juu ya barabara. Hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
Mtu pekee aliyejeruhiwa katika ajali hiyo, alikuwa kwenye TOYOTA
Huko bondeni ndiko lilikotumbukia gari dogo (TOYOTA)
Kijana wa kimasai akiwa amebeba spika ya gari lililopata ajali
Gari lililopata ajali likiwa bondeni
Gari lililopata ajali likiwa limenasa kwenye miti
Baadhi ya abiria wakiwa wamepumzika wakisubiri uokoaji ukamilike waendelee na safari
Lori lililopata ajali na kusababisha ajali ya gari jingine likiwa katikati ya barabara
Dereva wa gari lililosaidia kuvuta lori lililopata ajali alidai alipwe pesa ndio atoe msaada huo, hapo akikabidhi pesa zilizochagwa na baadhi ya abiria ndipo aanze kazi ya uokoaji.
Haikuwa kazi rahisi kulivuta gari hilo
uokoaji wakamilika
Nondo zilivuta na gari pia abiria walizivuta kwa mikonoPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top