Jeshi la polisi kanda Maalum Dar es Salaam limewataka wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kutulia wakati madai yao ya kuhitaji ulinzi wao na mali zao kufuatia matukio ya kuporwa,kupigwa,kulawitiwa na kubakwa.
Hata hivyo kamanda wa kanda Maalum Dar es Salaam
Suleimani Kova amesema atayashughulikiwa madai hayo baada aya kuzungumza na
wanafunzi na wananchi wa kigamboni mazungumzo yaliyofanyika katika uwanja wa
Machava Kigamboni.
MATUKIO KATIKA PICHA YA MAANDAMANO YA WANAFUNZI IFM JIJINI DAR ES SALAAM
Wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa
fedha IFM wakiwa wamejazana kwenye kivuko huku wakigoma kushuka hata baada ya
kuamriwa kwamba kiusalama itakuwa vigumu kwao kusafiria kwenda kigamboni.
Hatimaye wanafunzi wa IFM wamekubali kushuka
na kupungua ili kuwapisha wengine na kuvuka kwa awamu kuelekea kigamboni
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia
akiwaagiza wanafunzi wa chuo cha uongozi wa fedha IFM kuelekea eneo la uwanja
wa Machava kwa ajili ya majadiliano lakini wanafunzi hao wakakataa na kuanza
kuongea maneno ya kashfa ndipo mabomu ya machozi yakawatawanya wanafunzi hao.
Baada ya mabomu ya machozi wanafunzi
wanajisalimisha kwa kunyoosha mikono juu.
Wanafunzi wakiruka kichura huku wengine
wakitembelea magoti
Wanafunzi wakipakiwa katika gari ya polisi
kuelekea kituo cha polisi Kigamboni
Wanafunzi wa IFM wakiwa chini ya
ulinzi wa jeshi la Polisi baada ya rabsha za hapa na pale kutulizwa.
Pata shika nguo kuchanika hapa
wanaonekana Wanafunzi wa IFM wakigombea wenyewe kuingia kwenye gari dogo la
Polisi kuelekea kituo cha Polisi Kigamboni.
Mwanafunzi wa kike ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiwa
ameanguka kufuatia kashkash baina ya jeshi la polisi na wanafunzi wa IFM
Mwanafunzi mwingine wa kike akisaidiwa
kuinuka baada ya kuanguka katika purukushani hizo.
Mwanafunzi akionekana hajiwezi baada ya
kukimbia na kuanguka mara kadhaa kwa mshtuko wa bomu.
Mwanafunzi mwingine akiwa hajiwezi akiugulia
maumivu baada ya misukosuko ya hapa na pale
Ni kama wanasema Makamanda tumekubali kurudi
meza ya mazungumzo,wanafunzi wakielekea kituo cha polisi Kigamboni kwa
mazungumzo na maafisa wa jeshi la Polisi.
Hapa mwenye kutembea kwa magoti haya mwenye
kusota kichura chura haya ili mradi wafike Kigamboni Police Post
Wanafunzi wa IFM wakiwa mbele ya Kituo cha Polisi Kigamboni
wakipewa maelekezo na hatimaye wakaelekea uwanja wa Machava kwa mazungumzo na
jeshi la Polisi.
Post a Comment