Taarifa
iliyotufikia inaeleza kuwa yule Dereva aliyemgonga askari polisi wa
usalama barabarani WP 2492 CPL-Elikiza na kutokomea, amekamatwa jana
usiku masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa askari huyo maeneo ya
Bamaga mapema jana mchana.
kwa
Mujibu wa kamanda wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani nchini,Kamanda
Mohamed Mpinga amesema leo kuwa gari lilohusika kwenye ajali hiyo
limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini Dar.
Kamanda
Mpiga ametoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete nyumbani
kwa Marehemu,hukoUnunio,kaskazaini mwa jiji la Dar. Rais Kikwete alifika
kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha Mume na watoto
watatu.
Post a Comment