Loading...

BUNGE LIMEAZIMIA KUPITISHA AZIMIO LA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA BUNGE TOLEO LA 2007 SEHEMU YA 9

Bunge-Tanzania
Kufuatia utekelezaji wa mchakato mpya wa upitishwaji wa Bajeti ya Serikali Bungeni itakayokuwa ikipitishwa kabla ya Julai Mosi ya kila mwaka, Bunge Limeazimia Kupitisha Azimio La Marekebisho Ya Kanuni Za Bunge Toleo La 2007 Sehemu Ya 9
Akiwasilisha mapendekezo hayo mbele ya Bunge, Naibu Spika wa Bunge JOB NDUGAI amesema kuridhiwa kwa marekebisho hayo yanayohusu utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha yatawezesha wabunge kupanga matumizi ya fedha kabla ya Bajeti ya Serikali haijapitishwa.
Akichangia hoja hiyo Mbunge wa Singida Mashariki Chadema ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni TUNDU LISSU licha ya kuunga mkono hoja hiyo amekitaka kiti cha Spika kuacha upendeleo kwani Bunge hilo ni la vyama vingi.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum CCM, ANNA ABDALAH ametumia fursa hiyo kuwataka Wabunge kuyatumia ipasavyo marekebisho hayo katika kuibana serikali.
Kabla ya marekebisho hayo hayajapitishwa, Spika wa Bunge ANNE MAKINDA amewataka Wabunge kujiandaa kwa kanuni hizo mpya ikiwemo kutupia muda wanaopewa kujadili masuala ya msingi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Tukisalia Bungeni imeelezwa kwamba Wakazi wa Jiji la Mwanza wanatarajia kuepukana na adha ya uvukaji wa barabara katika eneo la Mabatini – Nyamagana baada ya ujenzi wa daraja la juu la waenda kwa miguu linalojengwa na Kampuni ya Nordic Construction Ltd utakapokamilika.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi GERSON LWENGE amesema, mradi huo wa ujenzi utakaotekelezwa kupitia Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/14 utagharimu zaidi yak Shilingi Milioni 800 mara utakapokamilika.
Hata hivyo licha ya ujio wa daraja hilo Mbunge wa Viti Maalum MARIA IBESH HEWA ameonesha wasiwasi wake juu ya wakazi wanaoishi katika eneo utakapotekelezwa mradi kama watalipwa fidia.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top