Jackson Odoyo,Arusha
KIPIGO cha mabao 3-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Morocco kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam, imeipaisha timu ya Taifa ya Tanzania,
(Taifa Stars) kwa nafasi 3 zaidi.
Kwa muujibu wa viwango vya soka vilivyotolewa jana na Shirikisho la
Soka Ulimwenguni FIFA vimeipaisha Tanzania kutoka nafasi 119 mwezi
uliopita hadi nafasi 116 mwezi huu.
Tanzania ilianza kupanda katika viwango hivyo baada ya kuichapa
Cameroon kwa bao 1-0 kwenye uwanja huo huo kabla ya kukutana na Morocco
na kuishushia kipigo cha mbwa mwizi.
Mbali na Tanzania kupanda kwa nafasi hizo tatu bado imeshindwa
kuikamata Uganda inayoongoza kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki ikiwa
kwenye nafasi ya 92 huku Kenya ikiwa kwenye nafasi ya 122.
Namba moja imeendelewa kushikwa na Hispania huku mabingwa wa Kombe la
Mataifa ya Afrika Nigeria ikiendelea kuwa vinara wa Afrika na kushika
nafasi ya 30 duniani.
Post a Comment