
Ripoti hiyo licha ya kuonesha kuwa na mafanikio katika nyanja ya utawala bora ikihusisha usimamizi na uwajibikaji, imetiwa dosari na kitendo cha Serikali kuifuta iliyokuwa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma POAC na kazi zake kuhamishiwa kwenye Kamati ya PAC iliyo chini ya Uenyekiti wa ZITO KABWE.
Kufuatia hali hiyo Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, LUDOVICK UTOUH akiwa mjini Dodoma anakemea kitendo hicho kwani kitapunguza uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi.
Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC, ZITO KABWE amesema, kuanzia sasa atapendekeza misamaha yote ya kodi kutangazwa huku akisikitishwa na kitendo cha Wizara ya Nishati na Madini kushindwa kukusanya mirabaha katika baadhi ya migodi nchini.
Ripoti hiyo ya CAG pia imebainisha kutokuwa na utaratibu mzuri wa Bajeti ya Serikali kutokana na kutegemea asilimia 50 ya fedha kutoka kwenye makusanyo ya kodi mbalimbali wakati mwaka wa fedha unapoanza.
credits:http://www.cloudsfm.co
Post a Comment