Loading...

Kijana akamatwa kwa kuvunja mlango wa nyumba na kuiba pesa wilayani Songea

JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Philemon Komba (20) mkazi wa kijiji cha Sinai kilichopo wilaya ya Songea vijijini kwa tuhuma za kuvunja nyumba na kufanikiwa kuiba shilingi elfu sitini ambazo zilikuwa zimehifadhiwa chini ya godoro ambalo lilikuwa ndani ya nyumba hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma  Deusdedit Msimeki alisema kuwa tukio hilo lilitokea julai 21 mwaka huu majira ya saa 6 mchana huko katika kijijicha Sinai.

Alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Thobias Mtoro (26) mkazi wa kijiji hicho alivunjiwa nyumba na kuibiwa fedha taslim kiasi cha shilingi elfu sitini na Komba ambaye alikamatwa muda mfupi tu wakati akiwa anatoka ndani ya nyumba hiyo.

Alieleza zaidi kuwa inadaiwa Komba alivunja nyumba hiyo na kufanikiwa kuiba wakati mmiliki wa nyumba hiyo alikuwa shambani kuvuna mahindi na kwamba siku mbili kabla inadaiwa Mtoro alikuwa ametoka kuuza baadhi ya mahindi aliyokuwa nayo jambo lilomfanya mtuhumiwa Komba kuamua kwenda kuvunja nyumba hiyo akidhani kuwa angeweza kuzipata fedha nyingi zilizotokana na mauzo ya mahindi ya mmiliki wa nyumba hiyo.

Kamanda wa polisi Msimeki alisema kuwa mtuhumiwa Komba amekwisha kukamatwa na polisi inaendelea kumhoji zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapo kamilika.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top