Rehema Selemani (10) mwanafunzi wa shule ya msingi Majimaji iliyopo katika wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma amekufa maji baada ya kuzama wakati anaogelea kwenye bwawa la maji lililopo jirani na kambi ya magereza.
Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi Deusdedit Msimeki alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 11 jioni huko katika kijiji cha Majimaji kilichopo wilayani Tunduru.
Msimeki alisema kuwa sikuhiyo ya tukio Rehema akiwa na wanafunzi wenzake walikwenda kwenye bwawa la maji kuogelea ambako akiwa katikati ya bwawa ghafla alizama na baadaye wanafunzi wenzake walijaribu kumwoka ilishindikana.
Alieleza zaidi kuwa baada ya kutokea tukio hilo wanafunzi wenzake walipiga kelele kwa lengo la kuomba msaada ambapo watu walipofika kwenye eneo la tukio baadaye waliuona mwili wa Rehema ukiwa unaelea ndani ya bwawa hilo.
Alisema kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho Philemon Dastan alitoa taarifa juu ya tukio hilo kwenye kituo cha polisi cha Tunduru na askari polisi wakiwa wameongozana na mganga walifika kwenye eneo la tukio mara baada ya kupatiwa taarifa kuhusiana na tukio hilo ambako walifanikiwa kuopoa mwili wa marehemu Rehema na kwamba kwa sasa hivi polisi inaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo
Post a Comment