Loading...

Wanafunzi waingiliwa kimwili bila kujitambua -Songea

Joyce Joliga,Songea.
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea wameiomba Serikali kuwaongezea ulinzi kutokana na kuingiliwa na Wanaume nyakati za usiku.

Mkuu wa Wanafunzi katika shule hiyo Janemary Mwinyikombo alisema tabia ya kuvamiwa mara mara na wanaume imeongeza hofu ya wanafunzi na kusababisha kushindwa kujisomea nyakati za usiku.

Kiranja akiwa na Katibu Bernadetha Mathew pamoja na wanafunzi waliofanyiwa vitendo vya kinyama ikiwa ni pamoja na kuchaniwa nguo kwa wembe na mwanaume ajulikanaye kwa jina la Ankol .ambaye mara kwa mara huingia kwa njia ya kimazingira wamesema hali hiyo inawakosesha raha shuleni hapo.

Wamesema pamoja na wanafunzi kufunga milango na kupigilia misumari kwenye madirisha lakini cha kushangaza wanaume hao huingia na kuchana nguo za wasichana maeneo ya kifuani, wamesema hali hiyo hutokea kuanzia saa 7:00 usiku na pale wanapo ingia wanafunzi hukumbwa na hali ya kushindwa kusema.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Welinald Liwiki alikiri kuwepo kwa vitendo hivyo na kwamba ameongeza ulinzi, yeye mwenyewe pia anashiriki ulinzi, na ameiomba jamii kushirikiana na shule katika kuwafichua watu wanaofanya vitendo hivyo kwa wanafunzi.

Alisema wakati wakifanya doria shuleni hapo usiku alinusurika kuuwawa na mlinzi baada ya mlinzi kufikiri yeye ndiye mwanaume anayewaingilia wanafunzi kimazingira.

Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea kwa miaka miwili mfululizo imekuwa na vitendo vya wanaume kuwaingilia wanafunzi kimazingira ingawa hali hiyo bado ni tata, wanafunzi wameomba jamii na wazee wa mila kukaa na kulitatua tatizo hilo vinginevyo itasababisha wanafunzi kuathirika zaidi kisaikolojia na hatimaye kushuka kwa kiwango cha elimu.

chanzo mwananchi Agosti 20


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top