Na Steven Augustino,Tunduru
IMEELEZWA kuwa Serikali isipochukua hatua za makusudi kuzuia na kutuliza vitendo vya uchomaji wa mabanda ya Nguruwe,kuharibu mali za watu pamoja na kuchoma moto nyumba vinavyo endelea kwa siku tano mfululizo huenda wimbo wa amani na utulivu ambao umekuwa ukiimbwa kila pembe ya nchi yetu ukatoweka hususani maeneo ya Wilayani hapa.
Minong'ono na kauli za baadhi ya Wananchi kuanza kukosa uvumilivu imeanza kujitokeza kufuatia matukio hayo yanayo onesha kuhatarisha amani yanayo jitokeza mjini hapa huku vikundi vinavyo daiwa kutumia mwamvuli wa madhehebu ya Waislamu wenye msimamo mkali kuendelea kuvamia na kuchoma moto makazi ya watu na mazizi ya nguruwe.
Kwa mjibu wa matukio hayo katika kipindi hicho Jumla ya mazizi 24 yamelipotiwa kuteketezwa na moto ambao jumla ya nguruwe 61 wameuawa pamoja na kuunguza nyumba za makazi ya watu vyote vikakadiliwa kuwa na thamani kiasi cha zaidi ya milioni 11 vimehalibiwa na kuziacha familia husika zikirudi katika lindi la umasikini uliopindukia.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, waathirika wa matukio hayo ambao wanaishi mitaa wa Nakayaya,Tuleane na Xtended mjini hapa, Luka Victor na Casian Asenga walisema kuwa kikundi hicho ambacho kimekuwa kikifanya matukio hayo majira ya usiku wa manane na kuharibu mali kwa kuchoma mazizi na nyumba zao na kuua nguruwe wameharibu na kuvuluga mifumo ya maendeleo yao.
Nae Douglas Mwasimba alisema kuwa wahalibifu hao wa mali zake walivamia katika nyumba yake majira ya saa nane usiku wakati amelala na kwamba alisikia nguruwe wanalia kwa pamoja kilio kilichoashiria tukio lisilo la kawaida na alipoamka na kuelekea kwenye mazizi aliona moto mkubwa na tayari nguruwe wake 38 walikuwa wameteketea na moto huo huku nguruwe 51 wakiwa wamejeruhiwa kwa kuunguzwa na moto huo.
Akielezea kwa masikitiko makubwa Thomas Mumba muuzaji maarufu wa nyama ya nguruwe mjini hapa, alisema kuwa kikundi hicho usiku huohuo kilifika kwake mnamo saa tisa na kilifanikiwa kuchoma zizi na kuua nguruwe 3 na kuwajeruhi wengine 5. Nako kwa Godfrey Mgao nguruwe 4 wameuawa na 5 wamejeruhiwa. Aidha Kikundi hicho hakikuishia hapo kwani siku ya pili kiliendelea na kampeni yao hiyo hadi katika Mtaa wa Tuleane na kuchoma moto Mazizi ya Mradi wa Kanisa Angarikana wanaofugiwa katika nyumba ya mchungaji wa Kanisa Mch. Edwin Nakajumo pamoja na mazizi ya Afisa maendeleo ya Jamii Mary Ding'oi ambako walifanikiwa kuchoma mazizi na moto huo kudhibitiwa mapema.
Walisema inaonesha wazi walengwa wa matukio hayo ni Waumini wa madhehebu ya kikristo Siku ya tatu kikundi hicho kilirudi tena mtaa wa Nakayaya hadi kwa Mchungaji wa Kanisa La Biblia Mch. Yakobo Milanzi na -kufanikiwa kuchoma mazizi na kujeruhi nguruwe 8 Haikutosha kikundi hicho kilifika mbali zaidi kwa kutaka kuua watu usiku wa siku iliyofuata kikudi hicho kilifika na kuunganisha umeme (to shorten) kwa makusudi na kuiunguza nyumba na Mashine ya kusaga mali ya Godfrey Christopher pia walifanikiwa kuteketeza kwa kuchoma moto nyumba ya Jastene Severin Magwinda Walifanikiwa na nyumba hiyo iliwaka moto.
Haikuleta madhara kwa binadamu kwani wote waliolala humo walinusulika kifo kutokana na tukio hilo. Akizungumzia matukio hayo Mweyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Wilaya hiyo Chande Nalicho mbali nakukiri kuwepo kwa matukio hayo aliwahakikishia wananchi wa mji waTunduru na Wilaya kwa ujumla kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa hali ya usalama inarejea katika hali ya kawaida Aidha Dc,Nalicho aliendelea kubainisha taarifa yake kuwa tayari serikali imeandaa mikakati mbalimbali ya kuhakiksiha kuwa watuhumiwa wa matukio hayo wana kamatwa ili sheria iweze kufuata mkondo wake na akatumia nafasi hiyo kuwaomba Wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa kuwataja watuhumiwa kwa siri katika ofisi yake.
Loading...
Post a Comment